KUMBUKA NI WAPI ULIPOKOSEA UKATUBU

| Makala

 Changamoto nyingi ambazo tunakutana nazo leo hii katika maisha yetiu,zinatokana na aina ya maisha tuliyowahi kuyapuuzia na kuyachukulia kawaida.

Wengi wetu bila kujua madhara na hasara zake kiroho,tulikimbilia kwa waganga wa kienyeji pale ambapo tulikuwa tunahitaji msaada juu ya mambo fulani katika maisha yetu labda ni kwenye

•            Biashara

•            Ndoa

•            Uzao

•            Masomo

•            Kazini

•            Afya na mambo mengine kama hayo..

Kitendo cha kuanza kupiga hatua kwenda kwa mganga wa kienyeji maana yake unampungia Yesu mkono wa kumwambia yeye hawezi kukusaidia na umepata njia mbadala itakayokufaa.

Yesu huwa halazimishi na ndomana ametupatia wanadamu utashi,maana yake tunayo maamuzi na uwezo wa kuamua lolote kwenye maisha yetu.

Huenda tusikukataze kwenda kwa hao unaowaamini kuwa watakusaidia, lakini madhara yanapokupata na unaanza kumtafuta tena Yesu uliyemkataa mwanzoni,huenda itakugharimu mambo mengi sana ili kupona na kutoka katika vifungo vya giza,

Wengi huwa wanadhani tu kwamba wakienda kwa mganga basi watapewa wanayoyataka na kuondoka…HAPANA……Ule ni ulimwengu wa giza kumbuka na adui hawezi kukuacha tu kizembe umfuate mwenyewe na akuache uondoke tu,

Wote wanaokwenda kwa waganga huwa wanapandikizwa na maroho mengine yatakayokufuatilia wewe na kila kitu cha maisha yako, ili moyo wako ubaki kumtegemea mganga na madhabahu hiyo ya kipepo uliyoifuata,na ndomana kuacha kwenda huwa inahitajika nguvu nyingine ya juu zaidi kumshinda adui.

Utahangaika kuombewa kwenye kila madhabahu na kila mtumishi lakini bila kujua chanzo cha tatizo lako ujue hakuna uponyaji utakaoupata mpendwa.

Biblia inatuambia KUMBUKA NI WAPI ULIPOKOSEA UKATUBU….Maana yake bila kukumbuka ni wapi ulipotegwa na adui na ukamfuata yeye,hautapata msaada kamwe.

KUNA MAMBO KADHAA UNAYOYAHITAJI KUTOKA KWA YESU,KAMA WEWE NI MUHANGA WA TATIZO HILI…………Nitakufundisha zaidi madhabahuni, na hakikisha unafuatilia kwa umakini mkubwa sana sana, ili nawewe Yesu akuvushe hapo.

 


 SADAKA