KUNGURU MCHAWI NDOTONI:

| Makala

KUNGURU MCHAWI NDOTONI:

USHUHUDA:

Bwana Yesu asifiwe, Pastor nimefuatilia somo la ndoto mtoto aliyedonolewa na Kuku. 

Mimi niliota kunguru kaninyofoa nyama kwenye tumbo langu upande wa kulia chini ya kitovu..nilisikia maumivu makali sana hadi nilipoamka yale maumivu yalikuwa bado yapo. Sikuelewa kwa kuwa ilikuwa ndoto. Chakushangaza baada ya wiki nikaumwa sanaaa hosp wakasema ni mchafuko wa damu nikachomwa sindano na drips na dawa nyingi nikapewa baada ya siku tatu nikazidiwa na kupelekwa hosp nyingine ambapo ilikuwa usiku wa manane kufikishwa tu nikaambiwa appendex imepasukia tumboni 

harakati za operation zikaanza usiku uleule na hiyo appendex ni sehemu ile ile aliyonyofoa nyama kunguru, operation iliyopangwa kufanyika ndani ya saa moja na daktari moja tu, ilifanyika kwa masaa manne na madaktari wakaongezeka maana ilikuwa na maluweluwe mengi na madaktari hawakuamini kama kweli nime survive maana hali ilikuwa mbaya sana.

 siku nimeenda kutoa nyuzi wale madaktari wote walioshiri katika operation yangu walikusanyika wakasema tumshukuru Mungu kwa hili alilolitenda. 

Pastor hiyo ya operation ilifanyika mwaka jana November lakini hadi leo upande ule wa operation umevimba. Naomba msaada wa kiroho maana sidhani kama ni issue ya kimwili tena hii. Bwana Yesu asifiwe.

@sirizabiblia

Pastor Innocent Mashauri

+255 758 708804


 SADAKA