Makala
MADHARA YA KUSHINDWA KUJISAMEHE
| Makala
Kuhusu Kujisamehe mwenyewe:
Kwenye moyo wako zingatia sana usibebe mambo yaliyokuumiza na yamepita, Hata kama yalikuumiza kiasi gani,jitahidi sana yasiendelee kukutesa na kuyakwamisha maisha yako.
Huenda kuna maisha fulani ambayo sio mazuri ulikuwa unaishi, maisha yasiyompendeza Mungu wako, na hiki kitu kinakutesa sana pamoja na kwamba umeshampokea Yesu…..
Huenda kuna matukio yaliwahi kutokea na hayakuwa mazuri, yaliacha alama mbaya na yenye uchungu kwenye maisha yako, kila unapokumbuka hayo matukio moyo wako unaanza kuuma upya, ni kama unawekewa msumari wa moto kwenye kidonda kibichi.
{ulifukuzwa kazi, uliachika,ulifeli,ulifiwa na mtu wa karibu,ndoa iliharibiwa na mtu wa karibu,nk}
Yote hayo yanaweza kuwa sababu ya wewe kuendelea kubeba maumivu kwenye maisha yako, na kwa bahati mbaya sana wengi wenu mnaanza kuwavujishia damu watu ambao hawakuwajeruhi.
“Kujisamehe ni zawadi unayojipatia mwenyewe”
Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema
{Warumi 12:21}
Somo linaendelea kwenye post inayofuata…….
Pastor Innocent Mashauri
Madhabahu ya SIRI ZA BIBLIA
Maarifa ya kiMungu
+255 758 708804
SADAKA