MAJANGA YA OCTOBER,NOVEMBER NA DECEMBER 2025:

| Makala

MAJANGA YA OCTOBER,NOVEMBER NA DECEMBER 2025:

MWENYE SIKIO NA ASIKIE.

Kuna mambo kadhaa ambayo muovu ibilisi amekusudia kuyatekeleza kwenye maisha ya watu wengi sana katika hii miezi mitatu iliyobaki ya kuukamilisha mwaka 2025,na Roho Mtakatifu ametoa maelekezo sahihi juu ya maeneo ya kuombea ili kuwa salama na kuepukana na majanga ya huu uovu uliopangwa kutokea kwa watu.

Huenda wewe ni mmoja wa watu waliokusudiwa kukumbwa na kimbunga hiki cha uovu kwenye maisha yako,nani ajuaye!! Na ndio maana nipo hapa very serious kukushirikisha jambo hili na kukukumbusha kuzingatia suala la maombi kwa kipindi chote cha kukamilisha huu mwaka tulionao.

Tunafahamu wazi kabisa kuwa roho Mtakatifu ndiye anayejua namna sahihi ya sisi tunavyotakiwa kuomba mbele za Baba yetu aliye mbinguni, na ndio maana biblia inajaribu kufafanua kwenye kitabu cha Warumi sura ya 8:26-27 inasema “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu”

Roho Mtakatifu hajataka tuhangaike kwenye maombi na kuomba maombi yasiyo na shabaha yeyote kiroho, ametupatia maelekezo madhabahuni,ni jukumu lako sasa kuzingatia haya maelekezo na kuchukua hatua madhubuti na ya kimkakati kuhakikisha unasimama kwenye nafasi yako na kupambania cha kwako ambacho adui amekusudia kukiharibu na kukiondoa kwenye maisha yako.

Kuna vitu viwili ambavyo Roho Mtakatifu ametuonyesha kuwa yatupasa kuvishughulikia sana na kuvilinda kwa maombi ya mara kwa mara kwa miezi hii ya kukamilisha mwaka 2025,vinginevyo alichokikusudia adui kutimia kwako basi utashuhudia kikitimia.

Sidhani kama utakuwa na sababu ya kumlalamikia Mungu endapo mambo yako yataharibika pamoja na kujulishwa maarifa haya mapema.

Mwenye sikio na asikie,tukutane Madhabahuni tuendelee na maombi ya KULINDA na KUTUNZA vya kwetu,mkono wa adui usipate nafasi yeyote ile kugusa wala kushika maeneo haya mawili tuliyoelekezwa kuyaombea.

Tuungane kwenye Post inayofuata ili tuyafahamu hayo mambo,na pia nikusaidie katika hatua za kuyaombea hayo mambo yako ili yasiguswe na adui shetani.

Tuwasiliane kupitia +255 758 708804 kama unahitaji ushauri wa kiroho,maombi na maombezi, ulimwenguni kote tunakufikia.

Youtube Channel {SIRI ZA BIBLIA}

Pastor Innocent Mashauri

Madhabahu ya SIRI ZA BIBLIA

Maarifa ya ki-Mungu


 SADAKA