Makala
MUNGU HAJIBU MALALAMIKO,ANAJIBU MAOMBI
| Makala
ACHA MALALAMIKO:
{MALALAMIKO SIO MAOMBI}
Na chochote ambacho sio maombi na hakina maombi ndani yake,hakiwezi kupatiwa majibu.
Jaribu kuangalia muda unaoutumia kulalamikia maisha yako na changamoto unazokutana nazo,halafu angalia muda unaoutumia kuyaombea maisha yako. Utagundua kuwa ni muda mwingi sana unautumia kulalamika juu ya maisha yako na mambo yako ambayo hayajakaa sawa kuliko kuomba.
Hakuna malalamiko yanayojibiwa na Mungu,na Mungu pia hapendezwi na walalamikaji.Sifa mojawapo ya mtu anayelalamika - huwa hana moyo wa shukrani kabisa,na Mungu hawapendi watu wasio na shukrani.
Ukisoma kitabu cha Habakuki utashangaa sana kwa habari ya hiki ninachojaribu kukuelimisha hapa. Habakuki alikuwa ni mtu wa malalamiko huenda kama wewe unavyolalamika juu ya mambo yanayoendelea kwenye maisha yako.
Sura ya kwanza ya Habakuki, inamuonyesha Habakuki akimlalamikia Mungu kwa mambo mbalimbali yanayoendelea.
Sura ya pili ya kitabu cha Habakuki,inayonyesha majibu ya Mungu yanayompa maelekezo ya nini cha kufanya ili aachane na kulalamika.
Mungu hakujibu malalamiko ya Habakuki,alimjibu alivyolalamika ili aachane na kulalamika.
Sura ya tatu ya Habakuki,tunaona kuwa habakuki halalamiki tena kama sura zilizopita. Sura hii Habakuki anafanya sala na maombi sasa.
Hiki kitabu ni kifupi sana na kimebeba maana kubwa sana kwenye maisha yetu ya kila siku.
Mungu hajibu malalamiko yako, anajibu maombi unayomuomba.
Ondoa malalamiko kwenye maisha yako,wekeza maombi kwa bidii na utaona matokeo.maana hii ndio sababu kubwa ya kwanini watu wengi hawajibiwi maombi yao!!!
Kile usichokitaka kwenye maisha yako, kibadili. Kama hakibadiliki, basi badilika wewe.
Chochote usichokibadili - umekikubali.
+255 758 708804 namba ya ushauri wa kiroho,maombi na maombezi
Pastor Dr Innocent Mashauri
Maarifa ya ki-Mungu
Madhabahu ya SIRI ZA BIBLIA
SADAKA