USIPUUZIE MANENO YA ADUI YAKO, FUTA HARAKA KWA DAMU YA YESU:

| Makala

USIPUUZIE MANENO YA ADUI YAKO, FUTA HARAKA KWA DAMU YA YESU:

Huenda ulikuwa haufahamu kabisa kwanini wakati mwingine maisha yako yanakwama mahali.

Najaribu kukupa ukweli ambao utakusaidia kwenye maisha yako, ile hali ya kutamkiwa maneno maovu,mabaya na ya laana kwenye maisha yako halafu wewe unachukulia kawaida kana kwamba hayatatokea kwenye maisha yako, ndugu yangu nakupa tahadhari mapema…..

Kila neno linalotoka kwenye kinywa cha mtu yeyote huwa na nguvu nyuma yake, na hiyo nguvu huwa inapewa sapoti na ulimwengu wa roho ili kilitimiza hilo neno lililotamkwa…..

Na ndio maana wakati Mungu anatamka kuhusu uumbaji kwenye kitabu cha Mwanzo mwanzoni pale, unatakiwa utambue kuwa alikuwepo Roho Mtakatifu na alikuwa ametulia juu ya vilindi vya maji, roho ndiye alikuwa anaratibu na kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawasawa na tamko la Mungu…..

U nani wewe unayetamkiwa maneno ya laana na unayachukulia kawaida, unamkumbuka yule dada tiktoker wa kenya aliyekuwa mjamzito? Unaikumbuka story ya maisha yake na nini kilimaliza uhai wake??

Mtu wa mungu nisikilize nikwambie, haya maisha tunayoyaishi yanaongozwa na kutawaliwa na ulimwengu wa roho ambao kwa macho ya nyama hatuuoni. Acha kuyaishi maisha yako kiukawaida,utachelewa sana kufanikiwa na huenda usifanikiwe kabisa…

Maana sikuhizi tuna watu ambao wako tayari kukuchukia hata kama hawakujua na hawajawahi kukutana na wewe na hamjakoseana popote pale, lakini wanaweza kukuchukia ukashangaa!!!!

Ndio maana narudia kusema kuwa,ukiamua kuokoka okoka kwelikweli na mpende Mungu sana ili uwe na bima ya uhakika ya ulinzi wa kiMungu maishani mwako.

USIPUUZIE MANENO YA ADUI YAKO, FUTA HARAKA KWA DAMU YA YESU:

Tuwasiliane kama kuna hitaji lolote unalotaka tumwambie Mungu kwa ajili yako, tuma meseji au voicenote kwa Whatssap namba +255 758 708804

Pastor Innocent Mashauri

Madhabahu ya SIRI ZA BIBLIA

Maarifa ya ki-Mungu


 SADAKA