Makala
VIKAO VYAO VYA USIKU WA MANANE
| Makala

VIKAO VYAO VYA USIKU WA MANANE:
Mara zote waovu ambao huwa wanazalisha maovu kwenye maisha ya watu,huwa wana vikao vyao vya makubaliano na vile vya kugawana majukumu ya siku,wiki,mwezi na hata mwaka na miaka, na wakati mwingine wanapeana assignment ambayo mpaka ilete matokeo ndio wamalizane na wewe.
Haya mambo yapo na yanaendelea vizuri sana kwenye ulimwengu wa roho katika giza, kwa bahati mbaya ni kwamba watu wengi hasa wakristo wamekuwa wakidhani kuwa kila kinachotokea kwenye maisha yao,kinatokea kwa sababu inabidi kitokee,au labda Mungu amekipanga. Wakati Mungu anatengeneza MEMA, adui pia huwa anatengeneza MABAYA na yote haya yanaandaliwa kwa ajili yako.
Biblia inaposema kuwa “lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake” Mathayo 13:20 - alikuwa na maana ya kwamba, waovu huamka ili kukufanya wewe uendelee kulala na usiamke ili wafanye mambo yao kwenye maisha yako.
Maisha ya watu wengi sana, na nasikitika hata kusema kuwa na wewe huenda upo,mnapangiwa maisha ya kuishi na shetani,na hii inatokana na vikao vyao vya kimkakati ambavyo huwa wanavipanga kila siku kwa ajili ya kazi tatu za shetani ambazo zinajulikana na biblia imejaribu kufafanua hili katika kitabu cha Yohana 10:10 “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu;
KUIBA, KUCHINJA, KUHARIBU.
Na haya ndio matokeo ya vikao vya siri vya gizani ambavyo waovu huhakikisha wanakaa na kukujadili namna watakavyokuangusha.
Na kwasababu vikao hivi hufanyika gizani na nyakati za usiku zaidi,na hasa usiku wa manane, ndio maana hata wewe unashauriwa kuwa na ratiba ya maombi ya usiku maana maombi ya usiku yana kazi kubwa mbili,
Hii siri alipewa yeremia kwenye sura ya 1,mstari wa 10
“Yeremia 1:10
Tazama, leo nimekuweka juu ya mataifa na falme ili kungʼoa na kubomoa, kuharibu na kuangamiza, kujenga na kupanda.”
Katika maombi yako ya kila siku usiku,usisahau kupindua meza zao wanazotumia kukujadili wewe na mambo yako, usisahau kuvuruga viti vyao wanavyokalia ili kufanikisha vikao vyao, futa kwa damu ya Yesu kila ajenda na mada zote zinazokuhusu wewe na nyumba yako ambazo wamepanga kujadili na kutekeleza,wachafulie lugha zao,wasielewane na wasikubaliane katika mazungumzo yao…..
Zaidi sana omba kwa msingi wa andiko hili Zaburi 104:4
Huwafanya malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa moto wa miali.
Mungu akufanye kuwa mwali wa moto,wakikuona wauone moto,washindwe kukusogelea,na wakikusogelea washindwe kukugusa na wakikugusa waugue na kuteketea kabisa.
Mafundisho haya yanaendelea zaidi kupitia Youtube Channel ya SIRI ZA BIBLIA, Whatssap Group kwa namba +255 758 708804.
Pastor Innocent Mashauri
Maarifa ya ki-Mungu
Kusimama kwenye lango lako la majira na kupanga mambo yako vile unavyotaka yaende.
Kupangua kila silaha na mashambulizi yanayopangwa na kutumwa kwako kwa majira hayo
SADAKA